
BELLA SUGAR CRAFT



Maua yangu ya sukari
yanatengenezwa kwa upendo mkubwa
Sisi hapa Bellasugarcraft ni wataalamu katika mapambo ya keki kutumia maua ya sukari na modeli za sukari.
Inahitaji uvumilivu mwingi lakini mwisho hulipa pale unapotazama uumbaji mzuri ambao umetengeneza , inakufanya usijutie muda wako.Inaridhisha sana kutengeneza maua ya sukari yanayofanana kwa ukaribu sana na maua ya ukweli , na unayaunda kwa vile unavyoyaona kwa tafsiri yako ya macho na sio lazima yawe sawa kibaologia.
Inafurahisha sana kuweka tabasamu katika sura ya mteja wake kwa kumuundia ubunifu wa maridadi wa sukari anaouhitaji.
​
Tunatoa madarasa Tanzania na Ujerumani na pia mtandaoni kwa wasioweza kuhudhuria madarasa . Bonyeza kitufe hapo chini kuona vifaa vya kutengenezea maua sukari tulivyonavyo .
​
Kutana na Bellafrida
Mimi ni msanii wa sukari na mbunifu wa keki za kifahari . Pia ni mwanzilishi na Mkurugenzi wa Bella Sugar Craft LTD iloyoko Munich , Ujerumani .
​
​
Ninaunda keki maalaumu za kifahari zilizopambwa na maua ya sukari kwa zile nyakati spesheli kwa shughuli muhimu za maisha.
​
​
Ninatoa madarasa ya kikundi na ya kibinafsi katika sanaa ya ufundi wa sukari , yaani maua ya sukari & modeli za sukari.
​
