top of page

Darasa Kikundi

Madarasa yetu ni ya sanaa ya kutengeneza maua ya sukari kwa kutumia mikono , na inafaa kwa yoyote haijalishi kama wewe ni mpya hujui kabisa au una ujuzi kidogo na unataka kuboresha ujuzi wako juu ya sanaa hii.

 

Utajifunza kutengeneza maua sukari ya ajabu na kuvutia ambayo yatabadilisha kabisa muonekano wa keki zako na kuzifanya zionekana za kitaalamu kabisa.

 

Ni  nafasi nzuri ya kushiriki na kujifunza vile vile kukutana na  wasanii wengine wenye shauku ya hii sanaa na upambaji wa keki kutumia sukari kwa ujumla.

​

​

IMG_5379_edited.jpg

Katika darasa hili utajifunza :

​

  • Kutengeneza maua tofauti ya sukari .

  • Kushika , kupaka rangi na kutumia paste ya sukari .

  • Kutumia vifaa kama vikatio , vibonyezo , waya na vinginevyo kuyapa maua yako uhalisia wa ukweli.

  • Kutumia rangi ya unga na vimeremeto kuyafanya maua yako yaonekane hai .

  • Jifunze siri na maujanja ya kutengeneza maua yatakayokutofautisha na upinzani na uweze kujibiwa maswali yako yote ulioyonayo kuhusu fani hii na mwalimu.

Utaondoka kwenye darasa hili na mpangilio wa onyesho la maua mazuri uliotengeneza na ujuzi mpya uliojifunza utakaokuwezesha kutengeneza maua mengine nyumbani kwako.
bottom of page