top of page
IMG_7644.JPG

KUHUSU MIMI

Halo, jina langu ni Bellafrida, mbuni wa keki ambaye anapenda kutengeneza maua ya sukari kwa mapambo ya keki maalumu.Mimi ni mtanzania lakini kwa sasa ninaishi Munich , Ujerumani.

 

 

Kwa asili mimi ni msichana wa kifedha

( Shahada ya uzamili ( MBA ) ya Biashara ya kimataifa ) lakini nimekuwa nikivutiwa na kupendezwa na sanaa ya aina hii. Ninaona mchakato mzima wa kuunda ni wa ajabu na wa kushangaza.

 

 

Kwa hivyo miaka michache iliyopita niliamua kusoma sanaa hii na nilikuwa na bahati nzuri kuchukua masomo na kujifunza kutoka kwa wataalam  waliobobea zaidi huku Ulaya.

 

 

Kuishi huku kumenipa nafasi ya kuchunguza zaidi juu ya ulimwengu wa mapambo ya keki na sasa nataka kushiriki kile nilichojifunza na marafiki wengine wa 'keki deco'. Natumai kukuhimiza kufanikisha ndoto zako na malengo ya sanaa hii .

bottom of page